Friday, March 18, 2011

KARIBUNI WOTE KWENYE MKUTANO JMOSI MARCH 19,2011

Ndugu WaTanzania wote,
Tunawataarifu kwamba kutakuwa na mkutano siku ya Jumamosi tarehe  19 March 2011. Wiki iliyopita tulifanikiwa kupitia kanuni za mfuko na kufanya mabadiliko kutokana na mawazo ya wajumbe. Wiki ijayo ni zoezi la kuchagua viongozi wa mfuko. Tungependa kuhamasisha watu wote wajitokeze kugombea nafasi za uongozi na pia kama kuna mtu unapendelea awe kiongozi tunaomba uongee naye akiafiki basi ni lazima awepo siku ya uchaguzi hii inaendana na kanuni za mfuko.Vilevile kwa wale watakao jipendekeza kugombea nafasi za uongozi watapaswa kuwepo ndani ya ukumbi wa uchaguzi ili kujinadi kwa wanamfuko na kupigiwa kura kulingana na kanuni za mfuko. Mwanamfuko ataweza kupiga kura kuchagua viongozi baada ya kulipa ada ya mwaka na ada ya uandikishwaji (registration fee) Kulingana na kanuni za mfuko. Kwakulipa ada hizo kunafanya mwanamfuko kuwa hai na kumpa mwanamfuko haki ya kupiga kura kufuatana na kanuni za mfuko. Ada ya mwaka ni $40, na ada ya uandikishwaji ya $10 ambayo italipwa mara moja (one time registration fee); Ada hizi  zinabidi zilipwe zote kwa wakati mmoja, kabla ya zoezi la uchaguzi kuanza siku ya uchaguzi. Tafadhari unaombwa kujiandaa kwa malipo ya ada hizi siku hiyo ili kuzingatia kanuni za mfuko katika kupiga kura. 
MKUTANO UTAANZA,
  Saa:           Kumi na Nusu.  (4:30 PM)
 Mahali:     AMERICAN LEGION COLUMBUS

5475 SANDALWOOD BLVD, COLUMBUS , OH 43229


Agenda za mkutano wa March 19, 2011 ni kama ifuatavyo.

1.Kujiandkisha kuwa mwanamfuko
2.Wagombea kujinadi kwa wana jumuiya
3.Uchaguzi mkuu


Tafadhali sambaza ujumbe huu kwa WaTanzania wote.
Asanteni Mungu awabariki.
WILLIAM MWANDAMBO

No comments:

Post a Comment