Monday, February 21, 2011

Rapa Eve na Mchumba wake Teodorin Nguema Obiang mtoto wa rais dikteta wa Equatorial guinea


Mcheza sinema na rapa mashuhuri nchini marekani EVE amekuwa akijivinjari na mpenzi wake Teodorin mwenye umri wa miaka 37 ambaye ni mtoto wa rais wa nchi ya equatorial guinea.Baba yake anasifika kwa mauaji ya wapinzani wake na dikteta mkubwa.
Ili kumfurahisha mpenzi wake Teodorin alikodisha boti ya Billionea wa microsoft kwa dola za kimarekani laki saba $700,000.Eve alifurahi sana.
Teodorin pia ni waziri wa misitu,mazingira na nyumba  nchini kwao na wizara anazoziongoza zinanuka rushwa.Familia yao imejilimbikizia utajiri mwingi kutokana na biashara ya mafuta mpaka kufikia mabilioni ya pesa lakini wananchi wao wa kawaida wanahangaika kutengeneza walau $1 kwa siku.
Jamaa inasemekana anamiliki magari na majumba ya kifahari Africa kusini,london,los angeles pamoja na switzerland.Now that's a baller!

source:NY TIMES

No comments:

Post a Comment