Monday, February 28, 2011

MKUTANO WA MFUKO WA JUMUIYA KUSAIDIA MATATIZO YA WATANZANIA

Ndugu WaTanzania wote,
Kazi mliotutuma tumeikamilisha, mawazo yenu mlio tukabidhi siku ya Jumamosi, Tarehe 18, December 2010 tumeyafanyia kazi kwa kina. Tupo tayari kurudisha report kwenu. Kwa mantiki hiyo tunawataarifu kwamba kutakuwa na mkutano siku ya Jumamosi tarehe  12 March 2011 na week inayo fuata siku ya Jumamosi tarehe 19 March 2011.
  Saa:           Kumi na Nusu.  (4:30 PM)
 Mahali:     AMERICAN LEGION COLUMBUS

5475 SANDALWOOD BLVD, COLUMBUS , OH 43229

Agenda za mkutano wa  March 12, 2011 ni kama ifuatavyo.

1. Kupitia kanuni za mfuko
2. kupendekeza na kujipendekeza majina ya viongozi 
Baada ya kupitia kanuni tunaomba tujiandae kwa uchaguzi.

Agenda za mkutano wa March 19, 2011 ni kama ifuatavyo.

1.Kujiandkisha kuwa mwanamfuko
2.Wagombea kujinadi kwa wana jumuia
3.Uchaguzi mkuu

Tungependa kuhamasisha watu wote wajitokeze kugombea nafasi za uongozi na pia kufanikisha mikutano yote miwili.

Tafadhali sambaza ujumbe huu kwa WaTanzania wote.
Asanteni Mungu awabariki.
Wenu,
WILLIAM MWANDAMBO.

No comments:

Post a Comment