Saturday, February 5, 2011

Jinsi ya kufile Tax bure

Kufaili tax ni kitu muhimu sana hapa Marekani na unaweza kujikuta kwenye matatizo makubwa usipofaili Taxes.Kwa kifupi kufile tax ni wewe kutoa taarifa serikalini kiasi chote ulichotengeneza kwa mwaka mzima uliopita na kiasi ulichokatwa kodi na kama hukutengeneza kiasi kizuri,maana yake kama bado upo chini ya mstari wa watu maskini basi serikali inakurudishia pesa yako kidogo.

Process ya kufaili tax ni nzito na inagharimu sana sometimes mpaka $100.Hivi ndio jinsi ya kuepuka gharama.Kama wewe pato lako limetokana na kazi na sio biashara na huna vitu vingi vingi basi unaweza kufaili bure mwenyewe unahitaji vitu vifuatavyo na muda wako kidogo lakini ni rahisi sana.

1.W-2 forms and 1099-forms.
2.Kama una watoto unahitaji tarehe zao za kuzaliwa na SSN zao.
3.Nenda hapa http://www.irs.gov/efile/article/0,,id=118986,00.html  ,Halafu click "browse a list of freefile companies"  halafu chagua kampuni yoyote unayotumia.Mimi napendelea H&R Block pamoja na TURBO Tax.

4.Then click hiyo kampuni utakutana na button inakwambia "leave IRS website" itakupeleka kwenye website ya kampuni kwa mfano H&R Block itakupeleka mahali panasema "start your free file now".

5.Sign up, enter your information correctly.Kila box kwenye W-2 lina namba kwahiyo ingizo hiyo info ziendane na box number kwenye website ya H&R Block.

5.Mwishoni unaingiza bank account na routing number ili wakutumie pesa zako kama utarudishiwa chochote.

6.Its really that simple,Voila! you are now a tax file expert.

7.Remember siku ya mwisho ya kufile ni april 14.Utaratibu huo hapo juu ni kwaajili ya Federal tax return tu,nitawaelekeza baadae jinsi ya kufanya state na local income Tax.Inachukua muda wa wiki mbili hadi tatu kwa pesa kuingia benki.

8.Vitu muhimu vya kutosahau ili uweze kupata fedha nyingi, Earned income credit,Tuition credit,Child credit,Child care and child dependent credit.

FURAHIA MAVUNO YAKO.MUNGU AWABARIKI NYOTE.

No comments:

Post a Comment