Monday, December 20, 2010

Matokeo ya Mkutano wetu wa tarehe 18 desemba.

Kwa wale waliokosa kuwepo kwenye mkutano ninawajulisha tu mambo machache na ya muhimu katika mkutano mzima.
    1.Bado tunahaja ya kuandika katiba ambayo kila mwanajumuiya ataifurahia na kuiamini na kuiheshimu.

    2.Bado maelewano yanaendelea kuhusu bei ya kujiunga kama mwanachama.

    3.Mapendekezo ya uchaguzi wa viongozi na mgawanyo wa majukumu.

    4.Bado kuna majadiliano makali kuhusu mfuko na jinsi ya kuukuza uwe mkubwa.Wengine wamependekeza kuinvest kwenye majengo na mikopo.
    
     5.Malalamiko yalikuwepo kwamba mwamko wa masuala ya jumuiya kutoka kwa watu bado ni mdogo mno.

     6.Mkutano mwingine unapangwa kufanyika mwezi mmoja baada ya mkutano wa dec 18.

Saturday, November 27, 2010

Karibuni Watanzania wote mnaoishi columbus na popote pale duniani.

Hii ni blogu yenu kwa ajili ya mambo yenu yanayotokea kwenye jumuiya yenu.Baadhi ya mambo hayo ni kupeana matukio ya harusi,kufuzu vyuo vikuu na mashule mbali mbali,taarifa za usalama ,uhamiaji,misiba,na kadhalika.Ni madhumuni yetu kuendelea kupendana,kuheshimiana,kushauriana na kusaidiana kama wanajumuiya ambao tumetoka sehemu moja-Tanzania.